Licha ya kuwa miji inaitegemea sana vijiji katika kujiendeleza na mwishowe kujipatia maendeleo hasa ya kiuchumi, vijiji vimekuwa vikionekana kurudi nyuma siku baada ya siku.
Vijana wa ngazi ya cheeti katika Chuo cha Mipango na Maendeleo vijijni kanda ya ziwa kilichopo katika mkoa wa Mwaza(Institute of Rural Development Planning(IRDP-LAKE ZONE CENTER FOUND IN MWANZA REGION)) walipata kuyatizama maisha halisi ya kijiji cha Mwalogwabagole kilichopo katika wilaya ya Misungwi ambacho kina hali ambayo vijiji vingi hapa nchini Tanzania vinayo.
Katika ripoti waliyokuja nayo vijana hawa inayaonyesha matatizo yanayokikabiri kijiji hiki cha Mwalogwabagole na pia sababu mbalimbali zinazokwamisha maendeleo ya kijiji hiki licha ya juhudi ambazo selikali ya Muungano wa Tanzania inazichukua kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhakikisha kijiji hiki na vijiji vingine vinapata maendeleo.
Matatizo yanayokikabili kijiji cha Mwalogwabagole ambayo yameonekana kuvikabili vijiji vingine vingi vya hapa nchini Tanzania.
Tatizo la Miundombinu mibovu ya barabara na Mawasiliano ni kikwazo kikubwa kwa vijiji vingi kikiwemo kijiji cha mwalogwabagole ambacho wanakijiji wake wanategemea sana shughuli za kilimo, na uvuvi kwa kuwa kiko kando mwa ziwa Vikitoria. Miundombinu ni tatizo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya kijiji kwa kua wakulima hushindwa kuzimudu gharama za usafirishaji wa mazao yao ya shamba kutokana na gharama hizo za usafirishaji kuwa juu kwa kua barabara ni mbovu. Tatizo hili upelekea mazao kkushindwa kufika sokoni kwa mda na mara nyingine kutokufika sokoni kabisa.
Hali ya barabara
Kwa mujibu wa wanakijiji, walidahi kuwa barabara ni kikwazo kikubwa sana kwa maendeleo yao, kwa kua barabara zao uharibiwa sana hasa kipindi cha mvua.
Mazungumzo na wanakijiji.
Pia Mawasiliano ni tatizo kubwa jingine ambalo linapelekea wakulima kushindwa kujua taarifa za masoko ya bidhaa zao wanazozizalisha. Kwa maelezo ya wanakijijj, kijiji kina mtandao mmoja wa simu ambao nao sio wa uhakika.
Ukosefu wa nishati ya umeme ni tatizo kubwa jingine ambalo kijiji hiki cha Mwalogwabagole na hata vijiji vingine vinakabiliwa nalo. Ukosefu wa umeme ni tatizo kubwa ambalo linasababisha shughuli nyingi za kiuchumi zinazotegemea nishati hiyo kutokuwepo na ambazo pengine zingekuwa ni kichochezi kikubwa katika kuleta maendeleo ya vijiji.
Moja kati ya nyumba nyingi zisizokuwa na nishati ya umeme katika kijiji cha Mwalogwabagole
Matatizo mengine kama :-
- Matatizo ya kijinsia
- Ukosefu wa elimu ya uzazi wa mpango
- Elimu juu ya gonjwa hatari la UKIMWI
- Elimu juu ya utunzaji wa mazingira,
- Utawala bora na
- Rushwa, pia ni miongoni mwa matatizo yanayovikabali vijiji vingi na kupelekea kutokupatikana kwa maendeleo katika vijiji vingi kikiwemo kijiji cha Mwalogwabagole. Baadhi ya Wanachuo cha Mipango katika picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment